BENKI YA NBC YASHIRIKI MBIO ZA RUANGWA MARATHON 2024
By Wallpaper HD

BENKI YA NBC YASHIRIKI MBIO ZA RUANGWA MARATHON 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wasanii maarufu na wadhamini wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa. Benki ya NBC ilikuwa ni moja ya wadhamini muhimu wa mbio hizo.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (kushoto) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe (kulia) na Meneja wa benki hiyo tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda (katikati) wakishiriki mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (katikati alievaa kofia) akifanya mazoezi ya viungo sambamba na washiriki wengine wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika tukio hilo lililovutia washiriki takribani 5,000 wakiwemo viongozi wa serikali, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Hamiss Mwinjuma, wasanii maarufu na wananchi, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun akiongoza maofisa wengine wa benki hiyo katika kushiriki mbio hizo akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe na Meneja wa benki hiyo tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (katikati alievaa kofia) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo wakijipongeza na medali zao mara baada ya kushiriki mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Lindi, Ruangwa: Septemba 16, 2024 - Benki ya Taifa ya Biashara NBC imeshiriki msimu wa pili wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 huku ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za wadau wa michezo nchini kupitia ushiriki, ufadhili, ubunifu na utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za kifedha mahususi kwa wadau wa sekta hiyo.

Dhamira ya benki hiyo ni sehemu ya mkakati wake katika kuunga mkono jitihada za serikali na wadau hao katika kukuza vipaji, kujenga afya ya jamii na kuongeza fursa za ajira hususani kwa vijana pamoja kusaidia ufanikishaji wa agenda mbalimbali za kijamii kupitia hamasa ya michezo.

Akizungumza wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa mwishoni mwa wiki, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema nia ya benki hiyo ni kuendelea kuwa mdau mkubwa wa sekta ya michezo nchini sambamba na kutumia vema huduma zake za kifedha katika kuwasaidia wadau wa sekta hiyo muhimu.

“Ushiriki wetu kwenye mbio hizi za Ruangwa marathon ni wa namna mbili, kwanza tumeingia kama moja ya wadhamini muhimu wa mbio hizi na pia tumeungana na washiriki wengine akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wa serikali katika kukimbia mbio hizi sambamba na kushiriki matukio mengine yalioambatana na mbio hizi lengo likiwa ni kufanikisha agenda yake ambayo ni kuchochea maendeleo kupitia sekta ya afya, utalii, na michezo.’’ Alisema.

Katika tukio hilo lililovutia washiriki takribani 5000 wakiwemo viongozi wa serikali, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Hamiss Mwinjuma, wasanii maarufu na wananchi ilishuhudiwa, Meneja huyo wa Kanda akiongoza maofisa wengine wa benki hiyo katika kushiriki mbio hizo akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe na Meneja wa benki hiyo tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda.

“Tumekuwa tukizingatia sana agenda mbalimbali zinazoambatana na matukio haya ya kimichezo na hilo limekuwa likitupa msukumo mkubwa kushiriki, kufadhili na hata kuandaa matukio kama haya.’’ Alisema Bi Zubeider huku akitolea mfano mbio za NBC Dodoma Marathon zinazoandaliwa na benki hiyo kila mwaka jijini Dodoma zikilenga kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kuboresha afya ya mama na mtoto.

Zaidi kupitia udhamini wake kwenye Ligi Kuu ya NBC (NBC Premier League), Ligi ya Vijana na Ligi ya Championship benki hiyo pia imekuwa ikibuni na kutoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wadau tofauti wa mchezo wa mpira wa miguu nchini ikiwemo mikopo ya usafiri kwa vilabu na Bima ya Afya kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi.

Akizungumza baada ya mbio hizo, Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha mbio hizo ikiwemo benki ya NBC pia alionyesha kuridhishwa na mchango wa sekta ya michezo nchini katika kufanikisha jitihada mbalimbali zinazolenga kusaidia jamii ikiwemo afya.

Download Wallpaper